“Tukitaka kumuenzi Sheikh Hassan Mwalupa na Sheikh Abdillah Nasir, ni wajibu wetu kusomesha na kuhuisha kazi zao walizozifanya masheikh hawa.”
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Leo hii, Matuga, Kaunti ya Kwale - 26 Julai 2025, Sheikh Mkuu wa Jumuiya ya Kiislamu ya Shia Ithna Ashari Tanzania (TIC), Maulana Sheikh Hemed Jalala Mwakindenge, ametoa wito kwa Waislamu kuwaheshimu na kuwaenzi Maulamaa waliotangulia mbele ya haki kwa kusomesha na kuendeleza kazi zao.
Akizungumza katika hafla ya Khitma (Hauli) ya Marhumu Samahat Sheikh Hassan Ali Mwalupa iliyofanyika Matuga, Kaunti ya Kwale, Kenya, Sheikh Jalala alisisitiza kuwa:
“Tukitaka kumuenzi Sheikh Hassan Mwalupa na Sheikh Abdillah Nasir, ni wajibu wetu kusomesha na kuhuisha kazi zao walizozifanya Masheikh hawa.”
Amesema kuwa maisha na mafundisho ya masheikh hao yalijengwa juu ya msingi wa elimu, umoja, na jitihada za kuhamasisha jamii juu ya Uislamu wa haki. Aliwataka vijana na wanazuoni wa leo kuyaenzi haya kwa vitendo.
Katika Khitma hiyo, waumini kutoka maeneo mbalimbali ya Kenya na Tanzania walihudhuria na kutoa heshima zao kwa marehemu, wakikumbuka mchango wake mkubwa katika Tabligh, elimu ya dini, na malezi ya jamii kwa misingi ya Qur’ani na Ahlul-Bayt (a.s).
Your Comment